Canada kumrudisha Rwanda Mugesera

Haki miliki ya picha AP
Image caption Mugesera akanusha madai ya kuwaita Watutsi mende

Canada imeamua kumrudisha Rwanda mtuhumiwa wa mauji ya kimbari Leon Mugesera

Mahakama ya Canadian imekataa ombi la rufaa kutoka kwa mshukiwa huyo aliyepinga kurudishwa kwao Rwanda akisema hatapata haki nchini huko.

Mugesera anakabiliwa na mashtaka ya kutoa matamshi ya kuchochea genocide na uhalifu dhidi ya binadamu.

Inasemekana hapo mwaka 1992 mbele ya kilichokuwa chama tawala cha wahutu MRND anadaiwa kusema kwamba watusi wauawe akiwaita 'mende'.

Mwenyewe amekanusha madai hayo akisema matamshi yake yametafsiriwa vibaya.

Kwa mda wa miaka 16 amekuwa akipinga mahakamani hatua hiyo ya kumrudisha Rwanda akidai huko angeteswa au hata kuuawa.

Wakili wa Mugesera alikuwa ameomba apewe muda zaidi ili kamati ya umoja wa mataifa inayopinga vitendo vya unyanyasaji na mateso ichunguzi na itoe hakikisho kuwa hatapatwa na kadhaia hiyo lakini mahakama ilitupilia mbali ombi hilo.

Serikali ya Rwanda imefurahishwa na uamuzi huo.