AU yapata makao makuu mepya

Makao makuu mepya ya Umoja wa Afrika yamefunguliwa rasmi mjini Addis Ababa, Ehiopia.

Haki miliki ya picha AFP

Uchina ilitoa fedha kwa mradi huo uliogharimu dola milioni 200.

Jengo hilo lina mnara wa mita 100 mkabala na ukumbi mkubwa ya mikutano.

Waandishi wa habari wanasema jengo hilo kuwa ishara kubwa ya masilhai ya Uchina katika bara la Afrika.

Mkutano wa mwanzo wa viongozi wa Afrika kufanywa kwenye makao makuu mepya utaanza Jumapili. .