Mkurugenzi wa redio auwawa Mogadishu

Mkurugenzi wa redio ya binafsi nchini Somalia amepigwa risasi na kuuwawa mjini Mogadishu.

Haki miliki ya picha online

Tovuti ya redio na televisheni ya kituo Shabelle, imeeleza kuwa watu wawili waliokuwa na silaha walimuuwa Hassan Osman Abdi karibu na nyumbani kwake.

Haijulikani aliyefanya shambulio hilo.