Jumuia ya Kiarabu yashindwa Syria

Jumuia ya Nchi za Kiarabu imesimamisha shughuli za ujumbe wake wa uchunguzi nchini Syria.

Haki miliki ya picha AP

Kiongozi wa jumuia hiyo, Nabil el Arabi, alisema uamuzi huo ulichukuliwa kwa sababu ya hali kuzidi kuwa mbaya nchini humo, huku ghasia zikiongezeka.

Jumuia iliongeza muda wa safari ya ujumbe wake baada ya mwezi wa kwanza kumalizika, lakini nchi za Ghuba ziliondoa wachunguzi wao, na hivo kupunguza hadhi ya ujumbe huo.

Wanaharakati wanasema ujumbe huo haukufanikiwa.

Bwana El-Arabi amekuwa akizungumza na Warusi kujaribu kuwashawishi wasipinge azimio kuhusu Syria lilopendekezwa na nchi za Kiarabu katika Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa.