Afghanistan itazungumza na Taliban

BBC imepata taarifa kuwa serikali ya Afghanistan inapanga kukutana na Taliban nchini Saudi Arabia katika wiki chache zijazo.

Haki miliki ya picha AP

Mazungumzo hayo, ya mwanzo kati ya pande hizo mbili, ni muhimu katika juhudi za kutafuta suluhu ya amani katika vita vya Afghanistan.

Marekani hivi karibuni ilijaribu kuwasiliana na Taliban, ambao wako katika shughuli za kuanzisha ofisi nchini Qatar.

Rais Hamid Karzai wa Afghanistan, anasema mchakato wa kutafuta amani unafaa kuongozwa na Afghanistan yenyewe, lakini siku za nyuma Taliban iliidharau serikali yake kuwa siyo halali.