Wasunni Iraq waacha kususia bunge

Chama kikuu cha Wasunni nchini Iraq kinasema kitaacha kususia bunge, ili kusaidia kupunguza msukosuko wa kisiasa, ambao watu wengi wakiona unaweza kurejesha vita vya kidini.

Haki miliki ya picha Reuters

Chama cha Iraqiya kilisema hatua yao ni kuonesha nia njema kabla ya mazungumzo baina ya vyama vya siasa vya Wasunni, Washia na Wakurdi.

Lakini chama hicho kimesema kwa sasa, kitaendelea kususia baraza la mawaziri.

Msukosuko ulizuka mwezi uliopita baada ya waziri mkuu, Nouri al-Maliki, ambaye ni Shia, kutoa amri kuwa kiongozi mmoja wa Iraqiya akamatwe.

Wanasiasa wa Kisunni walimuelezea Bwana Maliki kuwa dikteta.

Mashambulio kadha ya mabomu dhidi ya maeneo ya Washia yalizidisha wasiwasi.