Ukame wa Sahel waathiri milioni 12

Rais mstaafu wa Ghana, John Kufuor, ameiambia BBC kwamba ukame katika kanda ya Sahel ya Afrika unaathiri watu kama milioni 12 katika mataifa ya Afrika Magharibi.

Haki miliki ya picha Reuters

Alisema ulimwengu haukujifunza kutoka yale yaliyojiri Somalia, na unasubiri hadi watu wafe kwa njaa kabla ya kutoa msaada wa kutosha.

Alieleza kuwa ukame unazusha mapambano nchini Ghana, baina ya wafugaji na wakulima:

"Tuna tatizo kubwa linaloendelea la wafugaji wanaohama kutafuta malisho.

Kila ukame ukikausha malisho katika Sahel, wafugaji wanaelekea kusini kwenye misitu, pamoja na Ghana.

Na siku hizi, kila ukifungua gazeti na kuskiliza redio, kila siku unasikia mapambano baina ya wafugaji wa kabila la Fulhani na wakulima."