Ajali yauwa mshauri wa Kabila

Mshauri mwandamizi wa Rais Joseph Kabila wa Jamhuri ya Demokrasi ya Congo, amekufa kwenye ajali ya ndege.

Haki miliki ya picha AFP

Mshauri huyo, Augustin Katumba Mwanke, alikufa pamoja na rubani, wakati ndege hiyo ya kibinafsi ilipuanguka karibu na mji wa Bukavu, kusini mwa nchi.

Waziri wa Fedha, Augustin Matata Ponyo, na abiria wengine walijeruhiwa vibaya.

Augustin Matata Ponyo, gavana wa Kivu Kusini, Marcellin Cishambo Rohuya, na mshauri mwengine wa rais, Antoine Ghonda, inaarifiwa waliumia vibaya.

Ndege hiyo ilikuwa inasafiri kutoka Kinshasa kuelekea Kivu.

Sababu ya ajali hiyo haijulikani.