Whitney Houston afariki dunia

Houston Haki miliki ya picha Redferns
Image caption Whitney amefariki akiwa na umri wa miaka 48

Mwanamuziki mashuhuri wa Marekani Whitney Houston amefariki dunia akiwa na umri wa miaka 48, kwa mujibu wa Kristen Foster, mwandishi wake wa habari.

Sababu za kifo chake na mahala alipofariki bado hazifahamiki, Bi Foster ameliambia shirika la habari la AP.

Akiwa mmoja wa wanamuziki wenye mafanikio makubwa duniani, pia aliwahi kuwa mcheza filamu, katika michezo kama vile The Bodyguard na Waiting to Exhale.

Fani yake iliwahi kuzongwa na matumizi ya dawa za kulevya na maisha yake yenye matatizo katika ndoa na msanii Bobby Brown.