Mawaziri Uganda wajiuzulu

Mawaziri wawili ambao waliamuliwa kuwajibika nakuisababbishia serikali hasara ya dola milioni 60, kutokana na malipo ya kufidia mfanya biashara baada ya kupoteza umilikaji wa soko kadhaa mjini Kampala,wamejiuzulu.Hii inatokana na mapendekezo ya tume iliyochunguza matumizi ya mali ya Umma.

Image caption Jengo la Bunge Uganda

Aliekuwa waziri aliehusika na masuala ya jinsia pamoja na waziri mwingine katika ofisi ya waziri mkuu Kiddu Makubuya si mawaziri tena. Kiongozi wa shughuli za serikali bungeni Genarali Moses Ali kabla ya mjadala ulioanza kwa agenda kuhusu wahusika hao wawili kuendelea. Generali Ali alisoma taarifa ya serikali kuhusu mapendekezo ya kamati ya bunge na kueleza kuwa wahusika wamekubali kuwajibika kisiasa, na kukubali kuwa walikosa na hivyo wakajiuzulu.

Bw.Khiddu Makubuya amesema kuwa kutokana na hayo anachukua uwamuzi wa kujiuzulu wadhifa wake kama waziri wa masuala ya jumla katika ofisi ya waziri mkuu.

Lakini mwenzake Syda Bumba aliekuwa waziri anayehusika na masuala ya jinsia licha ya kukubali kuwajibika kisiasa lakini anadai kuwa hana hatia kwa sababu aliyoyatenda alikuwa akifuata sheria ya kutekeleza mapendekezo ya mwanasheria mkuu.

Haya yote yamesababishwa na uchunguzi ulionza mwaka uliopita ambapo tume ya bunge ilikuwa ikichunguza hasara ya dola million 60 zilizopewa mfanya biashara Basajjabalaba ikiwa ni fidia kwake baada ya hasara aliyopata kutokana na kupoteza tenda ya masoko ya mjini Kampala.

Mfanya biashara huyo alipoteza Tenda ya kumiliki masoko hayo baada ya Rais kuamua kuwa masoko yote yasimamiwe na wananchi wa kawaida walio katika masoko hayo.

Kwa sababu hizo uwamuzi ulipitishwa Bw.Hassan Basajjabalaba alipwe fidia, lakini wabunge wanasema kuwa pesa hizo zilikuwa nyingi kupita kiasi. Mawaziri hao walidai kuwa walipokea maagizo kutoka kwa Rais ambaye hata hivyo aliwaruka alipofika mbele ya Kamati ya Bunge inayochunguza kashfa hii.

Hawa mawaziri ni watatu kujiuzulu katika kipindi cha miezi mitatu kuanzia mwezi Disemba mwaka jana.