Uchunguzi wa ugonjwa wa kusinzia

Maradhi huathiri watoto Haki miliki ya picha na
Image caption Maradhi huathiri watoto

Utafiti kuhusu ugonjwa usiojulikana chanzo wala tiba yake yaani wa kusinzia lakini usio kuwa wamalale baado unaendelea.

Ugonjwa huo unashambulia maeneo kadhaa ya kaskazini mwa Uganda ambapo watoto 3000 wameathirika na ugonjwa huo wa ajabu. Watafiti mjini Kampala wamesema kuwa hali hio ya kusinzia kuna uhusiano na degedege ingawa hadi sasa hakuna ishara kuwa unaambukiza.

Maafisa wa wizara ya afya ya Uganda pamoja na washirika wao kutoka kituo cha uzuiaji na udhibiti wa magonjwa cha Marekani cha CDC wamesema kuwa juhudi zao kutaka kujua chanzo cha ugonjwa wa kusinzia ambazo zilianza mwaka 2009 zinaendelea na bado hazijafanikiwa.

Japo hali kwa ujumla ni hivyo, lakini kuna hatua iliyofikiwa,kama alivyoeleza Mkurugenzi wa kitengo cha uzuwiyaji na udhibiti wa magonjwa dunia cha CDC na mtafiti mkuu kuhusu ugonjwa wa kusinzia Scott Dowell wa kituo cha CDC cha Marekani mbele ya mkutano uliofanyika katika ubalozi wa Marekani mjini Kampala.

''Kile ambacho tumegundua kufikia sasa ni kinachosababisha mgonjwa kusinzia huwa na shambulio la ghafla la maradhi. Kwa hivyo kuna dalili fulani tumepata na zitatusaidia kushughulikia hawa watoto.

Dr.Dowell aliendelea kusema kuwa,

Tuna imani kuwa tiba dhidi ya shambulio la ghafla itaweza kusaidia watoto hawa. Hata hivyo,mtaalamu huyo ameongeza kusema kuwa hawajui ni aina gani ya dawa itakayoweza kufanya kazi hiyo. Pia miongoni mwa hatua mpya ni kutafuta uwezekano wa ugonjwa wa kusinzia kuhusiana na kimelea parasiti kinachosababisha kupofuka macho.''

Uchunguzi unaoendelea unaonyesha kama ugonjwa huu ni ''sindromu' kama anavyoeleza Dr.Antony Mbonye, kamishna wa huduma za kiafya katika wizara ya afya.

Katika lugha ya kiutibabu,tunaposema kuwa kitu ni sindromu huwa ni mlimbiko dalili yaani huwa ni mkusanyiko wa dalili kadha wa kadha ambazo huashiria ugonjwa Fulani.Ndio maana tunsema inaweza kuwa matatizo ya kifafa,utapia mlo,inaweza ikwa maambukizi mengine ambayo tunachunguza, ambayo yanasabaisha ugonjwa huu wa kusinzia.

Wataalamu wanasema kuwa maradhi haya ambayo chanzo chake hakijatambulika unasemekana uko pia Sudan ya kusini pamoja na nchini Tanzania lakini hawakutoa ufafanmuzi zaidi.

Hadi sasa watoto 3000 wameathirika na wengine 200 kufariki katika eneo la Acholi katika wilaya za Kitgum, Pader na Lamwo zilizoko kaskazini mwa Uganda.