Maandamano Afrika kusini kupinga unyanyasaji

Image caption mavazi ya sketi

Wizara ya jinsia na haki za watoto huko Afrika Kusini hii leo iliongoza maandamano ya kulalamikia kitendo cha kuwanyanyasa wanawake kwa misingi ya mavazi.

Maandamano hayo yaliongozwa na waziri wa jinsia Lulu Kisingwana pamoja na kamati kuu ya chama tawala ANC.

Miongoni mwa visa vilivyojitokeza hivi karibuni ni cha wanawake wawili waliodhalilishwa na kuzomewa hadharani na kundi la wanaume waliowazunguuka.