Sudan Kusini yanyan'ganya raia silaha

Sudan imekuwa na tatizo la usalama tangu kupata uhuru mwezi wa July, mwaka jana.

Haki miliki ya picha spl arrangement

Maelfu wameuwawa katika mapambano baina ya makabila.

Jeshi la serikali linajaribu kufanya raia wasalimishe silaha zao, lakini siyo kazi rahisi.

Kikosi nambari 6 ndio kimepewa jukumu la kukabidhiwa silaha na raia kutoka maeneo muhimu ya nchi.

Jimbo kubwa kabisa la Sudan Kusini, Jonglei, ndilo lenye matatizo zaidi.

Maelfu wameuwawa mwaka uliopita, katika jimbo hilo peke yake, katika mapigano ya kulipiza kisasi ya mara kwa mara baina ya makabila.

Zoezi la kuchukua silaha kutoka kwa raia miaka michache iliyopita halikufanikiwa, na lilifanya jeshi kuzidi kutoaminiwa na raia.

Kamanda wa kikosi nambari 6, Meja Marial Chanuong, anasema safari hii ni tofauti, na wana hakika raia watasalimisha silaha zao kwa wakuu.

Inakisiwa raia wana silaha nyingi kudhinda jeshi la Sudan Kusini, kwa sababu ya vita vya miaka mingi.

Ikiwa raia bado wana bunduki za rashasha, haitowezekana kuzuwia makabila kupigana.

Lakini kusalimisha silaha siyo rahisi.

Watu 74 waliuliwa katika jimbo la Warrap mwezi uliopita, na wavamizi kutoka jimbo la Unity, lilioko jirani.

Warrap ilisalimisha silaha, lakini Unity ilikuwa bado.