Serikali ya Senegal yaomba radhi raia

Haki miliki ya picha
Image caption Maandamano Senegal

Serikali ya Senegal imeomba radhi kwa kosa la polisi walioshabulia msikiti kwa gesi ya kutoa machozi, huku maandamano yakiendelea mjini Dakar dhidi ya rais wa nchi hiyo Abdoulaye Wade anayetaka kuwania urais kwa muhula wa tatu.

Mtu mmoja aliuawa mnamo Jumapili baada ya maandamano ya kupinga kitendo cha polisi kushambulia msikiti kwa gesi ya kutoa machozi siku ya Ijumaa.

Kwa mujibu wa vyombo vya habari nchini humo, watu sita sasa wameripotiwa kuuawa tangu kuanza kwa maandamano hayo ya kumpinga rais Wade.

Licha ya maandamano hayo hata hivyo rais Wade atagombea urais katika uchaguzi mkuu utakaofanyika Jumapili.