Mugabe atimiza miaka 88

Sherehe za kuadhimisha Rais Robert Mugabe wa Zimbabwe kutimiza umri wa miaka 88, zimefanywa katika mji wa Mutare, mashariki mwa nchi, na maelfu ya watu wamehudhuria.

Haki miliki ya picha BBC World Service

Matawi ya chama cha ZANU PF cha Rais Mugabe, yalichanga kugharimia sherehe hizo ambazo piya zilikuwa na mashindano ya warembo na mechi ya mpira.

Aliwaambia wafuasi wake kwamba wale wanaopinga msimamo wake dhidi ya wapenzi wa jinsia moja na ndoa kati yao, wapotelee mbali.

Bwana Mugabe alikanusha kuwa ni mgonjwa, na mapema juma hili alisema yeye kakazana kama kigongo na anaweza kuongoza nchi..

Umri wake pamoja na taarifa kuwa Rais Mugabe anauguwa saratani ya kibofu, imezusha wito mwengine kuwa Zanu PF inafaa kubadilisha uongozi.

Lakini chama chake kimemuunga mkono agombee tena urais mwaka huu.