Villas-Boas ahofia hatma yake

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Meneja wa Chelsea Andre Villas-Boas ahofia hatma yake

Kocha wa Chelsea Andre Villas-Boas amekiri kwamba anahofia majaaliwa yake katika klabu hiyo.

Villas-Boas, mwenye umri wa miaka 34, siku zote amesisitiza kuwa anaungwa mkono na mmiliki wa Chelsea Roman Abramovich.

Lakini katika mahojiano na kituo kimoja cha redio cha nchini Ureno anasema huenda akatimuliwa kama Carlo Ancelotti, ambaye alifutwa kazi mwezi Mei mwaka jana.

"Sijui kama nitakuwa hapa kesho au miaka miwili kutoka sasa, inategemea mtu anaelewa vipi hali ilivyo" alisema Villas-Boas.