Ujumbe wa misaada wazuiwa kuingia Baba Amr

Image caption Msafara wa misaada kutoka Msalaba Mwekundu wazuiliwa kuingia Baba Amr

Shirika la Msalaba Mwekundu limenyimwa kibali cha kusambaza misaada Baba Amr nchini Syria.

Hii ni wilaya katika mji wa Homs nchini Syria ambao umeshambuliwa kijeshi na vikosi vya serikali licha ya ruhusa ya awali iliyotolewa na mamlaka ya nchi hiyo.

Rais wa ICRC Jakob Kellenberger alisema kuzuiliwa huko ‘hakukubaliki.’

Kucheleweshwa huko kumessababisha tuhuma kuwa vikosi vya serikali vilikuwa vinajaribu kuondoa ushahidi wa mauaji yliyofanyika.

Baba Amr imeathirika vikali na mashambulio makubwa ya vikosi vya serikali katika wiki za hivi karibuni.

Baraza la Waasi nchini Syira (FSA) lilisema Alhamis kuwa linajitoa katika wilaya hiyokama‘mbinu ya kimkakati’

Ijumaa ofisi ya Umoja w Mataifa kuhusu haki za Binadamu ilisema imepokea muhtasari wa mauaji yaHomsya watu 17.

Waandishi wawili wa Ufaransa waliojeruhiwa kwa mabomu walitoroshwa kutokaHomskuingiaLebanonwamesafirishwa kurudiParis.

Rais wa Ufaransa Nicolas Sarkozy atakutana na waandishi hao Edith Bouvier na William Daniels watakapowasili.