Mitt Romney ashinda majimbo sita

Mitt Romney Haki miliki ya picha Getty

Mgombea wa urais wa chama cha Republican Mitt Romney ametwaa ushindi katika mchujo wa kinyang'anyiro kumtafuta mgombea rasmi wa chama hicho ambao ulifanyika majimbo kadhaa.

Romney amepata ushindi katika majimbo sita likiwemo jimbo lake la Massachusseta, Idaho, Vermont na Virginia.Alipata ushindi finyu eneo la Ohio sawa na Alaska.

Rick Santorum ametwaa majimbo kadhaa huku Newt Gingrich akishinda jimbo la nyumbani la Georgia. Mitt Romney ameweza kupata idadi ya wajumbe 415 wanaohitajika kumuidhinisha katika kongamano kuu la chama cha Repulican mwezi Agosti.

Licha ya ushindi wa Romney, wapinzani wake wakuu wameapa kuendelea na mchujo katika majimbo yaliyosalia. Bw Santorum, anaungwa mkono na wafuasi wakihafidhina ambao wanapinga ndoa za wapenzi wa jinsia moja na kuavya mimba.

Hata hivyo msimamo wake dhidi ya mpango wa uzazi wa kutumia dawa huenda umempokonya wafuasi walio na msimamo wa kadri.