Al-Shabaab yauwa wanajeshi wa Ethiopia

Kikundi cha wapiganaji wa Kiislamu nchini Somalia, cha al-Shabab, kimefanya shambulio dhidi ya wanajeshi wa Ethiopia na wa serikali ya Somalia, na kuuwa wanajeshi kadha.

Al-Shabaab walivizia na kushambulia kambi ya jeshi kwenye njia inayounganisha mji wa Baidoa na mpaka. Mapambano yaliendelea kwa saa nne.

Waandishi wa habari wanasema mapigano yalikuwa makali kabisa kutokea tangu wanajeshi wa Ethiopia kuingia nchini Somalia mwezi wa Novemba mwaka jana.

Al-Shabaab ilisema iliuwa wanajeshi 73 wa Ethiopia, lakini serikali ya Somalia inasema wapiganaji 45 walikufa.