Annan amekutana na Assad

Katibu Mkuu wa zamani wa Umoja wa Mataifa, Kofi Annan, amekutana na rais wa Syria, Bashar al-Assad, katika mji mkuu, Damascus.

Haki miliki ya picha Reuters

Mazungumzo yao yalichukua zaidi ya saa mbili.

Bwana Annan piya amezungumza na Waziri wa Mashauri ya Nchi za Nje, Walid Al Muallem.

Lengo la ziara yake hiyo ni kulifanya jeshi la serikali na wapiganaji kusitisha mapigano, na waanze kuzungumza.

Lakini makundi ya upinzani yanasema wakati wa mazungumzo umeshapita.

Taarifa ambazo haziwezi kuthibitishwa zinaeleza kuwa mji wa Idlib ulipigwa sana mizinga, muda mfupi kabla ya Bwana Annan kuwasili nchini humo.