Al-Qaeda wauwawa Yemen

Wakuu wa Yemen wanasema mashambulio makubwa kadha ya ndege yameuwa wapiganaji kama 18 wa al-Qaeda, kusini ya mji mkuu, Sanaa.

Haki miliki ya picha bbc

Inasemekana kuwa viongozi kadha wa wapiganaji waliuwawa.

Mashambulio hayo yalianza jana, ambayo mashahidi wanasema yaliendelea kwa kama saa mbili.

Ripoti zinasema mashambulio mengine yamefanywa leo.

Mashambulio yalilenga vijiji kwenye milima ya jimbo la Baida, ambako wapiganaji wenye uhusiano na al-Qaeda wamezidisha nguvu zao wakati wa ghasia nchini Yemen.