Japani yakumbuka tetemeko

Raia wa Japani walikaa kimya kwa dakika moja kukumbuka siku kama ya leo mwaka mmoja uliopita ambapo tetemeko la ardhi na tsunami lilikumba kaskazini mashariki mwa nchi hiyo.

Haki miliki ya picha no

Shughuli za usafiri zilisimama huku wananchi wakiwakumbuka takriban watu 20,000 waliokufa au kupotea kwenye maafa hayo.

Janga hilo pia lilisababisha miale ya nuclear kuchiririka kutoka kinu cha umeme cha Fukushima na kupelekea Japani kufikiria upya sera zake za nishati.

Mfalme Akihito na Waziri Mkuu Yoshihido Noda waliongoza maombi ya kitaifa mjini Tokyo.

Mfalme alisema kuwa Japani haifai kusahau majanga yaliyoikumba iwapo inataka kuwa taifa salama na lilostawi katika siku za usoni.