Sudan wapatana kuhusu mipaka na uraia

Salva Kiir na Omar al Bashir Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Viongozi hawa watakutana tena mjini Juba

Makubaliano hayo kati ya wawakilishi kutoka jamhuri ya Sudan and ile ya Sudan Kusini ni njia moja ya kuimarisha uhusiano kati ya majirani hawa ambao ulikuwa unazorota kwa kasi.

Nchini zote mbili zimekubaliana kuwa raia wao wataruhusiwa kuishi, kutembea na hata kuwekeza au kununua mali bila vikwazo vyovyote.

Makubaliano haya yatakuwa afueni kwa raia wa sudan kusini kama nusu milioni hivi, ambao bado wanaishi Sudan.

Utawala mjini Khartoum ulikuwa umetangaza kuwa kwanzia mwezi ujao, watalazimika kubadilisha uraia wao au watachukuliwa kama raia wa kigeni.

Mpatinishi mkuu katika mazungumzao hayo aliyekuwa rais wa Afrika Kusini Thabo Mbeki, amesema Rais Salva kiir na mwenzake Omar Al Bashir watatia saini makubaliano hayo katika sherehe rasmi itakayo fanyika Juba, mji mkuu wa Sudan Kusini.

Hata hivyo suala la mafuta ambalo limezua utata zaidi kati ya majirani hao bado halijatatuliwa.

Wawakilishi wa pande zote wamekubaliana kuhusu kutengeza mipaka kati yao.

Suala la kutokuwepo na alama za mipaka limekuwa likichochea mzozo kati ya nchi hizo mbili.

Hatua hii nu muhimu sana katika ile hali ya kuondoa hofu ya kuzuka kwa vita kati ya majirani hawa.

Hata hivyo wadadisi wa siasa wanasema bado ni mapema sana kusheherekea kwani mara kadhaa makubulaiano yaliotiwa sahihi hayajafuatiwa na utekelezaji.