Chama cha MMD Zambia chapata pigo

Chama kilichotawala Zambia kwa miongo miwili hadi kiliposhindwa kwenye uchaguzi uu mwaka jana, kimeondolewa uwezo wake wa kisheria.

Msajili mkuu wa vyama, nchini humo, amesema kuwa chama cha Movement for Multi-Party Democracy,(MMD) hakijawahi kulipia pesa za usajili tangu kuundwa kwake.

Chama hicho kinadaiwa takriban dola elfu sabini na tano. Wakuu wa chama hicho wanajiandaa kukata rufaa dhidi ya umauzi huo walioutaja kama kejeli kwa demokrasia.

Ikiwa kesi yake ya rufaa itatupiliwa mbali, huenda chama cha MMD, kikapoteza nafasi za wabunge wake bungeni.

Chama cha MMDkilingia mamlakani mwaka 1991, baada ya nchi hiyo kutupilia mbali utawala wa chama kimoja.