Ocampo amtaka Ntaganda

Image caption Generali Bosco Ntaganda

Luis Moreno Ocampo anasema kua Bosco Ntanganda lazima akamatwe na ahamishiwe kwenye korokoro za ICC mara moja.

Yeye anatakiwa kwa kuwasajili, kuorodhesha na kuwatumiaaskari watoto wakati wa mapigano ya wenyewe kwa wenyewe huko Ituri.

Bw.Ocampo anasema kua upande wa mashtaka unapanga kuongezea mashtaka mengine ya mauwaji na ubakaji kwenye waranti ya kumkamata.

Kwa wakati huu Bw.Ntanganda yuko katika Jeshi la Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo kama Jenerali.

Mwanasheria huyo amesema kua ulimwengu hauwezi kukaa kitako huku washukiwa wa uhalifu wakiendelea kuishi huru miongoni mwa umma.

Bw.Ocampo ana mipango ya kumtembelea Rais Kabila mwezi ujao kujadili jinsi ya kumkamata Bosco Ntaganda na kumfikisha huko The Hague.