Miripuko mjini Damascus yauwa watu kadha

Wakuu wa Syria wanasema miripuko miwili mjini Damascus imeuwa askari wa usalama na raia.

Haki miliki ya picha Reuters

Televisheni ya taifa imesema majengo ya ujasusi na usalama yamepigwa na milipuko hiyo, ambayo huenda ilitokana na mabomu yaliyotegwa kwenye magari.

Picha za televisheni zilionesha viungo vya miili, damu na magari na majengo yaliyovunjika.

Wakuu wamewalaumu magaidi kwa mashambulio hayo, na wadadisi kwenye televisheni walizilaumu Saudi Arabia na Qatar, ambazo zinaunga mkono upinzani.

Hakuna aliyedai kuhusika na miripuko hiyo.

Wanaharakati wa upinzani siku za nyuma wameishutumu serikali kufanya mashambulio kama hayo ili kuonyesha kuwa inapigana na magaidi.