DRC yatuhumiwa kwa mauaji ya raia

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Afisaa wa uchaguzi DRC

Vikosi vya usalama katika Jamuhuri ya Kidemokrasia ya Congo, vilifanya mauaji wakati wa uchaguzi mkuu chini humo mwishoni mwa mwaka jana.

Hii ni mwa mujibu wa ripoti ya umoja wa mataifa. Vikosi hivyo pia vinatuhumiwa kwa visa vya kuwakamata watu kiholela.

Ripoti hiyo ilitolewa na ofisi ya haki za binadamu ya umoja huo ikituhumu jeshi, polisi na vikosi maalum vya usalama kufanya mauaji mengine ya watu 33 .

Hata hivyo, waziri wa sheria wa nchi hiyo amekanusha madai hayo.

Wachunguzi wa kimataifa walielezea kuwa uchaguzi uliofanyika Novemba mwaka jana, rais Joseph Kabila akiwa mshindi, haukuwa huru na wa haki.

Ripoti hiyo ilizingatia matukio ya kati ya tarehe 26 Novemba na 26 Decemba mwaka 2011 mjini Kinshasa, eneo ambalo lilionekana sana kuunga mkono Upinzani.