Kaka wa Merah ahojiwa Ufaransa

Jaji anayehusika na kesi za ugaidi mjini Paris, anamhoji kaka ake Mohamed Merah, kijana aliyeuwa watu 7 kwenye mji wa Toulouse, Ufaransa, katika mfululizo wa mashambulio.

Haki miliki ya picha Reuters

Abdelkader Merah anaweza kukabili mashtaka ya kula njama na nduguye.

Bwana Merah amesema hakujua mpango wa mauaji hayo, lakini alisema anamuonea fahari ndugu yake.

Polisi walimpiga risasi na kumuuwa Mohammed Merah mjini Toulouse Alhamisi baada ya kumzingira kwa saa 30.