Mwenye bahati atafutwa

Mshindi wa kitita kikubwa kabisa cha bahati nasibu anatafutwa katika jimbo la Maryland, Marekani - kitita cha dola zaidi ya nusu bilioni.

Haki miliki ya picha Getty

Wakuu wanasema tikiti tatu zina nambari iliyobahatika; na washindi wako katika majimbo ya Maryland, Kansas na Illinois.

Inakisiwa Wamarekani walitumia dola bilioni moja na nusu kununua tikiti za bahati nasibu hiyo, ambayo imejilimbikiza kwa sababu hakuna mtu aliyeshinda tangu mwisho wa mwezi Januari.

Wakuu wanasema inaweza kuchukua saa kadha kuwapata washindi wa dola 640 milioni.

Aliyetangaza tikiti iliyoshinda alisema mshindi au washindi wanaweza kupata kitita kizima kwa pamoja, au kulipwa kiasi kila mwaka.

Vyovyote vile, mshindi lazima alipe kodi ya mapato.