Guruneti larushwa Mombasa

Mtu mmoja aliuwawa na wengine kama 20 kujeruhiwa kwenye mashambulio mawili ya maguruneti eneo la mwambao la Kenya.

Haki miliki ya picha 1

Ernest Munyi, mkuu wa mkoa wa mwambao, alisema mtu aliyekufa alikuwa kwenye mkutano wa hadhara wa Wakristo uliofanywa Mtwapa, kaskazini ya Mombasa, wakati guruneti liliporushwa kutoka gari iliyopita.

Alisema mripuko wa pili ulitokea kwenye mkahawa karibu na uwanja mkuu wa michezo wa Mombasa:

"Kumetokea miripuko miwili.

Moja hapa Mtwapa na moja huko Tononoka opposite Municipal Stadium.

Hapa Mtwapa mripuko uliotokea hapa ulirushwa kwa kikundi ambao walikuwa wakifanya maombi - ilikuwa Christian Crusade ikiendelea.

Kutokana na huo mripuko, watu 26 wamejeruhiwa na mtu mmoja amefariki.

Hiyo ndio habari ambayo tumepata sasa