Mapigano makali yatokea Somaliland

Mapigano makali yametokea Somalia baina ya wanajeshi wa eneo lilojitangazia uhuru la Jamhuri ya Somaliland na wanajeshi watiifu kwa eneo lilojitenga, liitwalo "taifa la Khatuma".

Haki miliki ya picha BBC World Service

Pande hizo zimelaumiana kwa kuanzisha mapigano hayo, ambayo yalitokea sehemu mbili (Las Anod na Buhoodle), kwenye eneo la mzozo la kaskazini-magharibi mwa Somalia.

Hospitali za huko zinasema kuwa watu kadha wameuwawa na kujeruhiwa.

Mwandishi wa BBC kwenye eneo hilo, anasema hayo ni mapigano makubwa kabisa kutokea tangu Khatuma kujitenga na Somaliland, awali mwaka huu.