Shambulio la kujitoa mhanga Afghanistan

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Athari za Mlipuko Afghanistan

Mshambuliaji wa kujitoa mhanga amejilipua na kusababisha vifo vya takriban watu kumi.

Inaarifiwa kuwa mtu huyo aliwalenga maafisa waliokuwa wanahudhuria mkutano mjini Maymana, mji mkuu wa jimbo la Faryab.

Zaidi ya watu 20 walijeruhiwa kwenye shambulio hilo,baadhi wakipata majeraha mabaya sana. Wengi wa wanajeshi wa kigeni mjini Faryab wanatoka Norway lakini msemaji wa jeshi la nchi alifahamisha vyombo vya habari kuwa wanjeshi hwakuwepo wakti wa shambulio hilo.

Mashambulizi kaskazini mwa Afghanistan, sio kitu cha kawaida ikilinganishwa na hali katika maeneo ya kusini na mashariki.

Jeshi la NATO lilithibitisha kuuawa kwa wanajeshi wake wawili katika mlipuko kaskazini mwa Afghanistan mapema leo ingawa hakuhusisha vifo hivyo na shambulio lililotokea mjini Faryab.

Hata hivyo jeshi halijatangaza majeruhi wa shambulio la Faryab.

Ingawa ilitangaza kwa upande mwingine kuhusu vifo vya wanajeshi wake watatu waliuawa hapo jana.