Maelf waandamana Mauritania

Rais wa Mauritania

Maelfu ya raia wa Mauritania wameshiriki maandamano katika mji mkuu Nouakchott,wakimtaka Rais Mohamed Ould Abdelaziz kuondoka madarakani.

Makundi ya upinzani yameongoza maandamano hayo ya amani kupinga kile wamesema sera za kiimla katika utawala wa sasa.

Bw Abdelaziz alichukua madaraka kupitia mapinduzi mwaka wa 2008 baada ya kuondoa utawala wa kidemokrasia.

Makundi ya upinzani yametoa taarifa ya pamoja kumtaka rais huyo aachie madaraka.Taarifa ya upinzani imeongeza kuwa rais wa sasa aliingia madarakani kinyume cha sheria wakimlaumu kwa wizi wa kura.

Rais Abdelaziz alipinga kufanya mazungumzo na upinzani punde baada ya kuchukua madaraka kupitia kura ya ghafla.

Kumekuwepo na maandamano ya mara kwa mara nchini Mauritania ambayo yanachochewa na wimbi la mageuzi linaloendelea katika nchi nchi za kiarabu.