Korea Kaskazini tiifu kwa kiongozi

Korea Kusini imezidisha shughuli za kutafuta mabaki ya roketi ya Korea Kaskazini iliyoshindwa kupaa hapo jana.

Haki miliki ya picha AFP

Korea Kaskazini kwenyewe kiongozi mpya, Kim Jong-un, amewapandisha vyeo maafisa 70, kuwa majenerali.

Na wanajeshi wengi walihudhuria mkutano mkubwa wa hadhara mjini Pyongyang.

Maelfu ya Wakorea Kaskazini walijaa kwenye uwanja wa michezo kusikiliza hotuba za kumsifu babu wa Bwana Kim, kiongozi wa kwanza wa taifa, Hayati Kim Il-sung, na kuonesha utiifu kwa kiongozi mpya, Kim Jong-un.