Wasudan wazozana tena

Mzozo wa mpakani baina ya Sudan Kusini na Kaskazini unazidi.

Haki miliki ya picha BBC World Service

Wakuu wa Sudan Kusini wamelishutumu jeshi la wanahewa la kaskazini kuwa limerusha mabomu kwenye soko, na kuuwa kama watu watano.

Shambulio hilo limetokea karibu na mji wa kusini wa Bentiu.

Hapo awali Sudan Kusini ilisema ilihimili shambulio la jeshi la Sudan Kaskazini, karibu na eneo la mafuta la Heglig, ambalo lilitekwa na wanajeshi wa Sudan Kusini Jumaane.

Serikali ya Khartoum haikusema kitu.

Mwandishi wa BBC anasema ugomvi ulioanza kama mzozo wa mpakani, umepelekea nchi hizo mbili kukaribia vita kamili.