Bashir,"Nitawakomboa raia wa S.Sudan"

Haki miliki ya picha BBC World Service
Image caption Wanajeshi wa Sudan Kusini

Rais wa Sudan Omar al Bashir The Sudanese president, Omar al Bashir, amesema anataka kuwakomboa raia wa Sudan Kusini kutoka kwa serikali yao kufuatia mapigano yanayoendelea kwenye mpaka kati ya nchi hizo mbili.

Rais Bashir alisema haya katika mkutano wa hadhara mjini Khartoum akisema mipaka kati ya nchi hizo mbili haiwezi tena kuheshimiwa.

Amesema wakati umefika kuamua ikiwa Sudan itasalia na Juba au Sudan Kusini kusalia na Khrtoum.

Aliitaja Sudan Kusini kama mdudu ambao unafaa kuangamizwa.

Mapigano kati ya nchi hizo mbili yamesambaa nje ya eneo la Heglig lenya visima vya mafuta na ambalo linadhibitiwa na Sudan Kusini.