Kamanda wa jeshi amshtaki Jack Staw

Haki miliki ya picha BBC World Service
Image caption Kamanda wa jeshi Abdel Hakim Belhadj

Mawakili wa kamanda wa jeshi nchini Lybia Abdulhakim Belhadj, wamewasilisha kesi dhidi ya aliyekuwa Waziri wa mambo ya nje nchini Uingereza Jack Straw.

Afisa huyo wa zamani anashtakiwa kwa kuidhinisha mpango wa kumkabidhi kamanda huyo kwa maafisa wa usalama katika utawala wa Muammar Gaddafi.

Bw. Belhadj anasema majasusi wa Marekani walimteka pamoja na mkewe wakati wakiwa safarini kuelekea Uingereza kutoka Malaysia.

Jack Straw alikuwa Waziri wa mambo ya nje wa Uingereza wakati wa tukio hilo.

Belhadj alianza kutayarisha kesi hiyo Disemba mwaka jana na duru zinasema Jack Straw amepokea nyaraka za mashtaka dhidi yake wiki hii.

Mlalamishi anadai Straw alishirikiana na watesi wake alipoidhinisha majasusi wa Uingereza kumkabidhi Belhadj kwa maafisa wa Libya. Jack Straw hajatoa taarifa kuhusiana na matukio ya sasa.