Breivik alipanga kulipua mabomu matatu

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Anders Behring Breivik

Anders Behring Breivik, mtu aliyewaua watu 77, katika mashambulizi mawili nchini Norway mwezi Julai mwaka jana, ameseme alikuwa na njama ya kulipua mamomu matatu yakiwa yametegwa kwenye gari.

Shambulio la bomu na ambalo ndio pekee alilokuwa ametega liliwaua watu wanane mjini Oslo.

Breivik alisema aliamua kuifutilia mbali njama yake ya mabomu matatu kwa sababu ya ugumu wa kuyatangeza kinyume na alivyokuwa amedhania.

Alipinga ripoti ya dakatari wa matibabu ya kiakili kuwa ana wazimu.

Mapema alifahamisha mahakama kuwa hakwenda kazini kwa mwaka mmoja , wakati huo wote akicheza mchezo wa kivita kwenye komputa wa "World of Warcraft" .

Aliarifu alivyokuwa akicheza michezo hiyo kwenye komputa na kujiifunza namna ya kutega mabomu kabla ya kulipua bomu lake la kwanza lililokuwa limetegwa garini mjini Oslo tarehe 22 mwezi Julai mwaka 2011.

Breivik alisema katika njama yake ya kulipua mabomu matatu alikuwa amelenga makao makuu yua serikali, ofisi za chama cha Labour pamoja na kasri la famialia ya kifalme, ingawa hakulenga familia yenyewe. Kesi ya bwana Breivik ingali inaendelea.