Mpalestina arejeshewa nyumba yake

Mahakama ya Israil yameamrisha kuwa familia sita za walowezi ziondoke kwenye nyumba katika mji wa Hebron, Ufukwe wa Magharibi.

Haki miliki ya picha

Mahakama yamesema nyumba hiyo bado inamilikiwa na Mpalestina.

Nyumba hiyo, ilio ubavu na eneo la makaazi ya WaIsraili, ilihamwa na Zecharaiah Bakri, baada ya jeshi la Israili kupunguza nyendo za Wapalestina katika eneo hilo.

Mhakama yaliamua kuwa nyaraka zilizotolewa na walowezi, kuonesha kuwa Bwana Bakri aliiuza nyumba hiyo, ni za uongo.

Waliamrishwa kulipa gharama zake za kesi.