Iran yaunda ndege isiyohitaji rubani

Iran inasema imeanza kuunda ndege ya ujasusi sawa na ile ya aina ya Sentinel ya Marekani, ambayo ilianguka nchini Iran mwaka jana.

Haki miliki ya picha Reuters

Wakuu wa Iran wanasema wamepata maelezo kuhusu namna ndege hiyo inavofanya kazi, kwa kufumbua fumbo la software yake; na sasa inaelewa kikamilifu muundo wa ndege hiyo.

Kuna wasiwasi kuwa Iran huenda ikaweza kuigiza rangi maalumu ambayo inasaidia kufanya ndege hiyo isionekane na vyombo vya radar.

Ndege hiyo ya aina ya Sentinel isiyohitaji rubani, inatumiwa sana na Marekani kugundua maficho ya makundi ya wapiganaji nchini Afghanistan na Pakistan.