Charles Taylor alifadhili Vita Sierra Leone

Imebadilishwa: 26 Aprili, 2012 - Saa 11:02 GMT

Hukumu dhidi ya Charles Taylor

Majaji wa mahakama maalum ya kimataifa wanatoa hukumu dhidi ya Rais wa zamani Liberia Charles Taylor.

Unahitaji toleo sahihi la Flash Player kucheza sauti/video

Cheza katika media player

Maelezo Live Usimulizi live kutoka BBC World Service.
Hii inajisasisha yenyewe.

Zindua

12:11: Jaji amesoma makosa yote 11 na kumuomba Taylor kukaa chini ambapo Charles Taylor amepatikana na hatia ya makosa hayo yote ya uhalifu wa kivita

12:09: Charles Taylor ameambia kusimama wakati hukumu dhidi yake ikisomwa

12:06:Mahakama imerejelea tena, ambapo majaji wa mamempata na hatia ya kufadhili uhalifu wakati wa vita nchini Sierra Leone.

Matangazo ya moja kwa moja yameahia kwa muda tu, hivi punde yatarejea.

11:56:Mahakama imempata na hatia Charles Taylor ya kufadhili  vitendo vya jinai nchini  Sierra Leone.

11:54:Jaji anasema mshtakiwa ilichangia kuimarisha harakati za waasi wa RUF ambapo aliwasaidia kwa hali na mali.

11:45:Mahakama inasema kuwa na ushahidi wa kutosha kwamba Taylor alitoa ufadhili wa kifedha kwa waasi wa RUF.

11:38: Mahakama inasema Japo Charles Taylor alikuwa na ushawishi kwa waasi wa RUF hakuwa na mamlaka yeyote katika usimamizi wa kundi hilo.

11:30: Mahakama imethibitisha kwamba Taylor alifahamu uhalifu uliotekelezwa na waasi wa RUF dhidi ya raia mwaka 1997 ambaoa lichukua hatamu za urais wa Liberia.

11:20:Jaji amesema uhusiano kati ya Charles Taylor na kiongozi wa RUF ulifanikisha mchakato wa amani nchini Sierra Leone. Hata hivyo amesema japo alichangia sana mazungumzo ya amani kuna wakati fulani alijaribu kuyumbisha mazungumzo hayo.

 

11: 15: Jaji amesema Taylor awapa waasi kambi ya mafunzo mjini Monrovia ambapo walipata silaha na kutoa almasi japo Taylor amekanusha hilo.

 

11:00: Jaji mwandamizi anasema kiongozi wa waasi wa RUF Foday Sankoh alikutana na Charles Taylor wakati wakifanya mafunzo ya kijeshi nchini Libya japo wawili hao walifanya bila kuingilia   mwingine.

 

10:45: Charles Taylor anahukumiwa na mahakama maalum ya Umoja wa Mataifa inayochunguza uhalifu wa kivita wakati wa vita vya muongo mmoja nchini Sierra Leone.Mahakama hii inafanya

vikao vyake The Hague, Uholanzi.

 

10:40:Takriban watu 50,000 waliuawa katika vita nchini Sierra Leone na maelfu ya wengine walikatwa viungo na waasi wa RUF ambao Charles Taylor anatuhumiwa kuwaunga mkono.

 

10:35: Jaji mwandamizi amesema upande wa mashtaka umethibitisha kwamba waasi wa RUF walitekeleza mauaji, ubakaji na kukata viungo vya raia wakati wa vita nchini Sierra Leone,

hata hivyo jaji hajasema ikiwa mahakama inamhusisha Taylor na uhalifu huo.

 

10:30: Taylor nakabiliwa na makosa 11 ya uhalifu wa kivita pamoja na dhuluma za kibinadamu

 

10:20: Charles Taylor ameshtakiwa kufadhili waasi katika nchi jirani ya Siera Leone ambapo amedaiwa kunufaika na madini ya almasi

 

10:09: Richard Lussick ndiye jaji mwandamizi wa kesi hii

 

10:05: Charles Taylor amekaa kimya wakati Jaji mwandamizi akianza kusoma hukumu

 

10:01:Mahakama ya kimataifa imeanza kusikiliza maamuzi dhidi ya Cherles Taylor

 

Taarifa zinazohusiana

BBC © 2014 Ilani: BBC haihusiki na yaliyoandikwa na tovuti za nje ya BBC.

Ukurasa huu unaonekana vyema kwa kivinjari cha kisasa kikiwa na laha mtindo (CSS).Wakati unaweza kuona yaliyomo katika ukurasa huu kwa kivinjari ulichonacho, hautaweza kufaidi kuona kila kitu vizuri. Tafadhali zingatia uwezekano wa kuboresha progaramu ya kivinjari au kuwezesha laha mtindo (CSS) endapo unaweza kufanya hivyo.