Mfalme Mswati apokea Ndege mpya

Wake wa Mswati
Image caption Wake wa Mswati

Mwaka wa 2002 mfalme HUYO alitaka kutumia fedha za umma kununua ndege yake binafsi, lakini juhudi hizo zikazimwa na maandamano ya umma.

Mfalme Muswati anaorodheshwa na jarida la Forbes akiwa wa 15 miongoni mwa falme tajiri duniani akiwa na mali inayokadiriwa kutimu dola milioni 100, huku raia wake wengi wakiishi kwa ufukara mkubwa.

Amelaumiwa kwa kuishi maisha ya anasa ingawa alisimamisha tamasha za kusherekea miaka 25 ya utawala wake mwaka jana kutokana na hali halisi ya Uchumi wa nchi yake.

Image caption Mfalme Mswati

Ndege mpya iliwasili Swaziland hapo Jumanne kama zawadi kutoka kwa wahisani na na marafiki wa Mfalme ambao hawakutaka kutambuliwa.

Msemaji wa serikali amekanusha taarifa kwamba ndege hii ni zawadi ya kusherekea siku ya kuzaliwa kwa Mfalme aliyetimiza umri wa miaka 44 hapo tarehe 14 Aprili.

Mnamo siku hiyo Machifu kote nchini Swaziland walitakiwa kutoa mchango wa ng'ombe wa kuchinjwa kwa ajili ya sherehe za kuzaliwa kwa Mfalme.

Vugu vugu la haki za binadamu ambalo huwashirikisha raia wa Swaziland nje ya nchi limepuzilia mbali maelezo ya serikali na kutaka kupata taarifa za kina kuhusu marafiki hawa waliojitolea kwa ukarimu wa kumzawadia Mfalme Mswati ndege.

Alipoulizwa ikiwa Mfalme Mswati alikaidi zawadi hiyo msemaji wa serikali Simelane amesema huwezi kuchunguza mdomo wa farasi uliyepewa kama zawadi.

Msukosuko wa kiuchumi unaokumba Swaziland umechochea maandamano ya kushinikiza kuwepo utawala wa demokarsia katika nchi ambapo vyama vya kisiasa vimefutwa.

Aidha nchi hii ndogo imetajwa miongoni mwa zile zenye idadi kubwa ya maambukizi ya virusi vya Ukimwi.