Burundi bado wasiwasi

Shirika la Human Rights watch lenye makao yake mjini New York Marekani, linasema kua ongezeko la ukiukaji wa haki za binadamu lilitokea nchini Burundi katika mwaka 2011.

Haki miliki ya picha BBC World Service
Image caption Mashambulizi ndani ya baa

Itakumbuka kua nchi ya Burundi ilijiondoa katika vita vya wenyewe mnamo mwaka 2005 baada ya miaka mingi ya mapigano lakini nchi hiyo inaendelea kukosa utulivu, kukiwa na mvutano baina ya makabila ya Wahutu na Watutsi.

Mhariri wa masuala ya Afrika Mary Harper amezungumza na mtayarishaji wa taarifa ya shirika hilo

Image caption nembo ya human rights watch

Human Rights Watch linasema kua watu wengi wameuawa katika mashambulizi yaliyochochewa kisiasa.

Linasema haliweza kutoa idadi kamili, lakini katika shambulio kubwa la hivi karibuni watu 37 waliuawa wakiwa ndani ya klabu ya pombe mnamo mwezi sebtemba mwaka jana.

Kundi hilo limeandika kikamilifu kile linachoelezea kua orodha ya walengwa wa kuuawa. Taarifa hio inaendelea kusema kua mwaka 2011 mauwaji yaliyo chagizwa kisiasa yalifanyika kwa kila wiki.

Mtayarishaji wa ripoti hio, Carina Tertsakian, anasema kua mauwaji ya wafuasi wa Chama cha upinzani chenye wafuasi kutoka kabila la Wahutu cha FNL yalikua ya kutisha.

Mauwaji yalifanywa sio tu kwa risasi moja bali mara nyingi mno. Kilikuepo kisa cha mwanachama wa FNL aliyepigwa zaidi ya risasi 30 kichwani.

Kulikuepo kisa kingine cha mtu aliyekatwakatwa, na kichwa chake kikapatikana mbali na sehemu nyingine za mwili.

Haki miliki ya picha other
Image caption Rais Pierre Nkurunziza

Shirika hilo linasema kua hata wanachama wa chama tawala wameuawa ingawa sio wengi.

Taarifa hio inaelezea mauwaji ya kulipiza kisasi, ambapo mwanachama kutoka chama kimoja huuawa saa chache baada ya mmoja kutoka chama kinachokinzana na hiki kuuawa.

Carina Tertsakian anasema kua tatizo ni kua mara nyingi hakuna anayekabiliwa na sheria.

Hata hivyo kuna hali ya afuweni, ambapo Polisi imeanza kufika mahali pa tukio na kuandika machache kuhusu tukio ingawa mambo huishia hapo.

Katika visa vingi familia zinasubiri washukiwa waliomuua mtu wao wafikishwe mbele ya vyombo vya sheria.