Guangcheng aondoka ubalozi wa marekani.

Mwanaharakati wa kijamii nchini China, mwenye ulemavu wa kuona, Chen Guangcheng, ameondoka kutoka ubalozi wa Marekani mjini Beijing, baada ya kukimbilia katika ubalozi huo, alipotoroka kifungo cha nyumbani mwezi uliopita.

Chen alisindikizwa na balozi wa Marekani, Gary Locke, kwenda hospitali mjini Beijing kwa uchunguzi wa kimatibabu.

Mke wa Bwana Chen na wanawe wawili nao pia wameondolewa kutoka jimbo lao la Shandong, Mashariki mwa China na kupelekwa katika ubalozi wa marekani.

China imeitaka Marekani kuiomba radhi kutokana na kitendo chake cha kuingilia masuala ya ndani ya nchi hiyo.

Hayo yamejitokeza wakati waziri wa mambo ya nje wa Marekani, Bi Hillary Clinton, akiwasili Beijing kwa mazungumzo na maafisa waandamizi wa serikali ya nchi hiyo