Naibu Waziri Mkuu, Kenya akihama chama

Haki miliki ya picha Getty
Image caption Musalia Mudavadi na Najib Balala

Naibu Waziri Mkuu nchini Kenya, Musalia Mudavadi amejiondoa kutoka chama chake ambapo pia ametangaza kuwania Urais mwaka ujao.

Bw Mudavadi ambae alikuwa mwandani wa Waziri Mkuu Raila Odinga na mmoja wa waanzilishi wa chama cha Orange Democratic Movement-ODM sasa amejiunga na chama kipya cha United Democratic Forum.

Pamoja na kujiondoa kutoka ODM, Naibu Waziri huyo amejiuzulu kama Waziri wa serikali za mitaa.

Akitangaza kujiuzulu kwake, Mudavadi amesema chama alichoamua kuwania Urais hakina sura ya kikabila.

Nchini Kenya machafuko ya kikabila yalizuka katika uchaguzi mkuu uliopita wa mwaka 2007.