Clinton akamilisha ziara yake-China

Hillary Clinton Haki miliki ya picha AFP
Image caption Hillary Clinton

Waziri wa mambo ya nje wa Marekani, Bi Hillary Clinton, ameondoka mjini Beijing baada ya kufanya mashauriano na viongozi wa taifa hilo.

Mazungumzo hayo yaligubigwa na mzozo kati ya mwanaharakati wa kijamii Chen Guangcheng na serikali ya nchi hiyo.

Mwanaharakati huyo bado angali anazuliwa katika hospitali moja mjini Beijing, licha ya tangazo la serikali ya nchi hiyo kuwa, Chen ataruhusiwa kuondoka nchini humo, kwa masomo zaidi.

Shirika la habari la serikali nchini humo, limeshutumu serikali ya Marekani, kwa kuingilia kati masuala ya ndani ya nchi hiyo, kufuatia uamuzi wa Marekani wa kuumpa Chen hifadhi katika ubalozi wake mwezi uliopita baada ya kutoroka kifungo cha nyumbani.

Mwanaharakati huyo mwenye ulemavu wa kuona, amesema anahofia usalama wake baada ya kuondoka kutoka ubalozi huo wa Marekani, lakini ameliambia shirika moja la babari nchini Marekani kuwa hataondoka nchini humo kwa muda mrefu.

Chen amepewa ufadhili wa kusoma katika chuo kikuu kimoja nchini Marekani.