Watu mia kadha wakamatwa Misri

Watu zaidi ya 300 wamekamatwa nchini Misri baada ya mapambano makali ya Ijumaa, baina ya waandamanaji na askari wa ulinzi, nje ya Wizara ya Ulinzi, mjini Cairo.

Haki miliki ya picha Reuters

Inaarifiwa kuwa mtaa huo sasa ni shuari, baada ya kafyu ya jana usiku kuondoshwa, lakini inaarifiwa kafyu itarejea tena usiku ya Jumamosi.

Mkuu wa Halmashauri ya jeshi inayoongoza nchi, Field Marshall Hussein Tantawi, amehudhuria mazishi ya mwanajeshi mmoja aliyeuwawa kwenye mapambano, yaliyozuka baada ya waandamanaji kujaribu kujivurumisha kwenye vizuizi ili waifikie wizara.

Ghasia hizo zimetokea kama wiki tatu kabla ya uchaguzi wa rais.