Vinu vya nuklia vyafungwa Japan

Kiwanda cha nuklia cha Fukushima Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Kiwanda cha nuklia cha Fukushima

Japan leo imezima mtambo wake wa pekee wa nyuklia unaofanya kazi, na kuacha taifa hillo kutokuwa na nguvu za umeme za atomiki, kwa mara ya kwanza kwa zaidi ya miongo minne iliyopita.

Wizara ya serikali za mitaa nchini humo, imekataa, kuruhusu viwanda hivyo kufunguliwa tena, licha ya wasi wasi kuwa huenda kukatokea upungufu na nguvu za umme nchini humo.

Serikali ya nchi hiyo inataka uzalishaji wa nishati ya atomiki kurejelewa lakini haitaka kulazimisha au kuharakisha shughuli hiyo.

Japan imekuwa ikiagiza gesi kutoka mataifa ya nje ili kukithi mahitaji yake ya nishati.

Hata hivyo kuna wasi wasi kuwa ukosefu wa nishati ya kutosha au kuongezeka kwa gharama ya nishati huenda kukaathiri secta ya viwanda nchini humo.

Vinu hivyo vya nuklia vimefungwa ili kuufanyia marekebisho ya kawaida.

Jumla ya vinu hamsini vya nyuklia nchini humo vimezimwa kwa muda.

Kumekuwa na wasiwasi kutoka watu wanaoishi karibu na maeneo yenye vinu vya nyuklia nchini humo, ambao usalama wao baada ya tukio la Fukushima.