Wasudan Kusini wajiandaa kurudi nyumbani

Maelfu ya Wasudan Kusini waliokuwa wakiishi kwenye pahala padogo kusini ya Khartoum, watarejeshwa Sudan Kusini.

Haki miliki ya picha Reuters

Shirika la kimataifa linalohusika na uhamiaji, International Organization for Migration, linasema limekubaliana na serikali ya Sudan kuwarejesha nyumbani Wasudan Kusini kama 15,000.

Watu hao wanategemea msaada wa chakula wa kimataifa, pamoja na maji na matibabu; na wengi wao hawana pesa za nauli.

Inakisiwa kuwa watu laki tatu na nusu kutoka Sudan Kusini bado wanaishi Sudan, ingawa walipewa muda hadi mwezi Aprili kusawazisha ukaazi wao Sudan, ama sivyo waondoke.