Serikali ya Uingereza yapata ujumbe

Nchini Uingereza, Waziri wa Fedha, George Osborne, ametetea sera za serikali baada ya chama chake cha Conservative kushindwa vibaya kwenye uchaguzi wa serikali za mitaa juma lilopita.

Haki miliki ya picha Reuters

Bwana Osborne, aliiambia BBC kwamba serikali imepata ujumbe, kwamba wapigaji kura wanataka serikali ishughulikie maswala muhimu kwao, kama ukosefu wa kazi, elimu na matibabu.

Lakini alisisitiza kuwa kurekibisha uchumi na kupunguza deni, ndio yanapewa kipa umbele.